Logo

    watoto

    Explore " watoto" with insightful episodes like "06 MACHI 2024", "Mtoto Charles: MONUSCO imenitoa msituni, asanteni sana", "WFP/UNICEF: Janga kubwa la njaa duniani linanyemelea Sudan miezi 11 baada ya kuzuka vita", "01 MACHI 2024" and "UNICEF Rwanda: Je wajua  kwamba watoto Rwanda wanaanza kupokea chanjo zao za kawaida karibu na nyumbani?" from podcasts like ""Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu", "Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu", "Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu", "Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu" and "Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu"" and more!

    Episodes (18)

    06 MACHI 2024

    06 MACHI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia mizozo na janga la kibinadamu nchini Sudan, na kuondoka kwa MONUSCO nchini DRC.  Makala inatupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Uganda, kulikoni? Takriban miezi 11 tangu majenerali wapinzani watangaze vita nchini Sudan, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa leo walionya kwamba mzozo huo unaweza kusababisha janga kubwa zaidi la njaa duniani.Harakati za ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, za kuondoka nchini humo zikiendelea, tunamulika hatua chanya zilizochukuliwa na ujumbe huo katika kunusuru vijana waliokuwa wanatumikishwa na waasi mashariki mwa nchi hiyo. Katika makala na tukielekea Siku ya Wanawake Duniani ambayo mwaka huu ina maudhui “Wekeza kwa wanawake: Harakisha maendeleo,”, tunatembelea wajasiriamali Kajiado nchini Kenya kusiki ni kwa jinsi gani wanawezakujiumudu kiuchumi.Na mashinani tunaelekea nchini Uganda kumsikia mkimbizi kutoka nchini Sudan Kusini.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

    Mtoto Charles: MONUSCO imenitoa msituni, asanteni sana

    Mtoto Charles: MONUSCO imenitoa msituni, asanteni sana
    Harakati za ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, za kuondoka nchini humo zikiendelea, tunamulika hatua chanya zilizochukuliwa na ujumbe huo katika kunusuru vijana waliokuwa wanatumikishwa na waasi mashariki mwa nchi hiyo.Miongoni mwao ni Charles, mwenye umri wa miaka 16 ambaye si jina lake halisi. Yeye alitumikishwa msituni na waasi kwa kipindi cha miaka miwili.Akizungumza huku sura yake ikiwa imefichwa kwenye video ya MONUSCO, Charles anakumbuka kuwa walikuwa shambani wanalima wakati waasi wa Mai Mai walipofika na kuwakamata.“Walitueleza kuwa hawana watu wa kuwasaidia mapigano hivyo wakatuchukua. Tulipofika walituona kuwa tuna mawazo ya kutoroka hivyo walitufungia ndani kwa wiki tatu,” anasema Charles.Anasema walipotoka fikra za kutoroka zikatoweka, wakafundishwa kupigana msituni na walipigana mara sita. Lakini haikuwa rahisi kwani wenzake 12 waliuawa huku porini wakati wa mapigano huku yeye mwenyewe akishuhudia.“Niliumia sana. Chakula nacho kilikuwa shida kupata, maisha yalikuwa magumu mno. Nikafikiria nikaona bora nirejee kwa familia yangu.’Walichofanya yeye na wenzake, usiku wa saa saba walitoroka hadi mji wa jirani ambako huko walijisalimisha kwa kiongozi mmoja na kumweleza kuwa wamechoka kuishi na kupigana porini.Kiongozi huyo aliwachukua na kuwapeleka Beni, mji ulioko jimboni Kivu Kaskazini.Charles anasema kiongozi huyo aliwasaidia kuwakutanisha na shirika la kiraia la ACOPE, mdau wa MONUSCO. Hapo walipata mafunzo kwa wiki tatu ikiwemo utengenezaji majiko banifu yasiyochafua mazingira.“Sasa maisha ni mazuri hapa na wito wangu kwa wale watoto na vijana walioko msituni wakipigana ni kwamba waondoke huko waache kupigana, waje wajisalimishe kwa serikali ili waweze kujiendeleza.”

    WFP/UNICEF: Janga kubwa la njaa duniani linanyemelea Sudan miezi 11 baada ya kuzuka vita

    WFP/UNICEF: Janga kubwa la njaa duniani linanyemelea Sudan miezi 11 baada ya kuzuka vita
    Takriban miezi 11 tangu majenerali wapinzani watangaze vita nchini Sudan, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa leo walionya kwamba mzozo huo unaweza kusababisha janga kubwa zaidi la njaa duniani. Sudan, nchi iliyo kaskazini mashariki mwa Afrika tayari iko katika mzozo mkubwa zaidi wa watu waliofuriushwa makwao duniani kwa mujibu, Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa, WFP.Na mapigano yanayoendelea kati ya Jeshi la Sudan SAF na kundi hasimu la msaada wa haraka RSF yamesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na wengine milioni nane kuyahama makazi yao ndani ya nchi na wengine kukimbilia nchi jirani.Hivi sasa watoto milioni 14 wanahitaji haraka msaada wa kuokoa maisha, limesema Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF katika tahadhari yale ya hivi karibuni, huku kukiwa na wasiwasi kwamba mzozo huo unaweza kuenea kwenye mipaka ya Sudan, na kutishia maisha na amani katika eneo hilo, endapo mapigano hayo hayatokoma.Cindy McCain, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa WFP amesema "Miaka ishirini iliyopita, Darfur ilikuwa janga kubwa zaidi la njaa duniani na ulimwengu ulijitolea kuchukua hatua. Lakini leo hii watu wa Sudan wamesahaulika. Mamilioni ya maisha ya watu, amani na utulivu wa eneo zima viko hatarini,” Bi. McCain ameyasema hayo akiwa Sudan Kusini, ambako amekutana na familia zilizokimbia ghasia na hali mbaya ya njaa Sudan na kuingia hiyo jirani zao. Amesema hivi sasa WFP inahaha kutimiza mahitaji ya chakula na kuongeza kuwa "Nimekutana na kina mama na watoto ambao wamekimbia Sudan ili kuokoa maisha yao sio mara moja, lakini mara nyingi, na sasa njaa inawanyemelea. Madhara ya kutochukua hatua yanakwenda mbali zaidi ya mama kushindwa kulisha mtoto wake na yataathili eneo hilo kwa miaka mingi ijayo”.WFP inasema leo hii chini ya mtu mmoja kati ya 20 Sudan ndiye anayeweza kumudu kupata chakula, watu 9 kati ya 10 wanakabiliwa na njaa  na mgogoro wa chakula umesambaa hadi nchi jirani zinazohifadhi wakimbizi wa Sudan na kuathiri watu zaidi ya milioni 25 Sudan, Sudan Kusini, na Chad.

    01 MACHI 2024

    01 MACHI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa 6 wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA6 unaokunja chamvi leo, na utafiti mpya uliotolewa leo na jarida la kitabibu la Uingereza Lancet na shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO kuhusu utipwatipwa. Mkutano wa 6 wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA 6 umefunga pazia leo jijini Nairobi, Kenya baada ya siku 5 za majadiliano na shughuli mbalimbali zilizohusisha zaidi ya wajumbe 7,000 kutoka Nchi 182 Wanachama wa Umoja wa Mataifa. Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini Nairobi UNIS, Stella Vuzo amekuwa akizungumza na washiriki mbalimbali kuhusu walivyonufaika na mkutano huo na hapa ni mmoja wao kutoka jamii za wafugaji ambao duniani kote mabadiliko ya tabianchi yanawaathiri moja kwa moja.Utafiti mpya uliotolewa leo na jarida la kitabibu la Uingereza Lancet na shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO unaonyesha kwamba, mwaka 2022, zaidi ya watu bilioni 1 duniani sasa wanaishi na unene wa kupindukia ama utipwa tipwa. Duniani kote, unene wa kupindukia kwa watu wazima umeongezeka zaidi ya mara mbili tangu mwaka 1990, na umepanda mara nne kwa watoto na vijana wenye umri wa miaka 5 hadi 19. Makala inaturejesha kwenye mkutano wa UNEA6 ambapo Viongozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa wamepata fursa ya kuwasilisha taarifa zao na kushiriki katika mjadiliano mbalimbali kwa lengo la kuisogeza dunia mahala bora zaidi katika upande wa mazingira. Stella Vuzo Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa Nairobi UNIS hakuachwa nyuma amekuwa akizungumza na wadau mbalimbali wanaoshiriki mkutano huo wa UNEA6 tangu ulipoanza na leo yuko na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) wa Tanzania Dkt. Selemani Jafo na kwanza amemuuliza anachokibeba kutoka kwenye mkutano huo.”Na mashinani tunamsikia binti Muthoni Truphena, kiongozi wa kikundi cha watoto wanaharakati wa mazingira nchini Kenya ambao wanachochea mabadiliko chanya katika jamii zao wakiungwa mkono na  Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira, UNEP, anapazia sauti kizazi chake katika mkutano wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA6 jijini Nairobi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

    UNICEF Rwanda: Je wajua  kwamba watoto Rwanda wanaanza kupokea chanjo zao za kawaida karibu na nyumbani?

    UNICEF Rwanda: Je wajua  kwamba watoto Rwanda wanaanza kupokea chanjo zao za kawaida karibu na nyumbani?
    Katika makala tunaangazia chanjo kwa watoto nchini Rwanda ambako Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaifadhili Rwanda Biomedical Centre (RBC) ambalo ni shirika kuu la kitaifa la utekelezaji wa afya lenye jukumu la kufanya utafiti wa kisayansi, kutoa huduma za uchunguzi, na kutekeleza afua za kiafya ili kulinda taifa la Rwanda dhidi ya magonjwa na matishio mengine ya kiafya. Anold Kayanda anasimulia.

    28 FEBRUARI 2024

    28 FEBRUARI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia msaada wa chakula nchini Sudan, na ulinzi wa amani katika jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini amabapo idadi ya wakimbizi imeongezeka. Makala tunakupeleka nchini Rwanda na mashinani nchini Kenya, kulikoni?  Msaada wa chakula cha dharura uliotolewa na Ukraine kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP kwa ajili ya operesheni zake nchini Sudan, leo umewasili katika bandari ya Port Sudan na kuapakiwa Kwenye malori tayari kwa kuwasambazia mamilioni ya watu wenye uhitaji wa haraka.Huku mzozo wa Sudan ukiendelea, wakimbizi na wanaorejea wanamiminika katika mipaka ya nchi jirani ya Sudan Kusini, wengi wamekuwa wakitafuta hifadhi katika jimbo la Upper Nile nchini humo na wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu.  Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umefanya mazungumzo na uongozi wa jimbo hilo kuona namna ya kuwasaidia. Makala tunaangazia chanjo kwa watoto nchini Rwanda ambako Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaifadhili Rwanda Biomedical Centre (RBC) ambalo ni shirika kuu la kitaifa la utekelezaji wa afya lenye jukumu la kufanya utafiti wa kisayansi, kutoa huduma za uchunguzi, na kutekeleza afua za kiafya ili kulinda taifa la Rwanda dhidi ya magonjwa na matishio mengine ya kiafya.Na mashinani tutaelekea nchini Kenya kusikia ujumbe wa mfugaji kuhusu uwekezaji katika sekta ya uzalishaji wa mifugo unaowezeshwa na Benki ya Dunia.Mwenyeji wako ni Evarist Mapesa, karibu!

    26 FEBRUARI 2024

    26 FEBRUARI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa sita wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA6 jijini Nairobi, na mradi wa kusaidia watoto na vijana ambao walikuwa na changamoto ya masikio na kuongea nchini Rwanda. Makala tunasalia nchin Kenya na mashinani ukanda wa Gaza, kuikoni?Mkutano wa sita wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA6 leo umefungua pazia katika Ofisi za Umoja wa Mataifa zilizopo jijini Nairobi, nchini Kenya. Mkutano huo utakaodumu kwa siku tano unahudhuriwa na washiriki zaidi ya 6000 ikiwa ni pamoja na viongozi wa Mazingira duniani, asasi za kiraia, wataalamu wa Mazingira, maofisa waserikali za mitaa, wakulima, vyama vinavyowakilisha wafanyakazi, jamii zilizoachwa nyuma pamoja na maofisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa.Kupitia mradi wa "Winsiga Ndumva", maneno ya lugha ya Kinyarwanda yanayomaanisha "Usiniache nyuma, ninaweza kusikia”, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na wadau wake ikiwemo Wizara ya Afya nchini Rwanda limebadilisha maisha ya watoto wengi na vijana ambao walikuwa na changamoto ya masikio na kuongea kwakuwapatia vifaa maalumu vya kupachika masikioni ili kusaidia masikio kufanya kazi yake ipasavyo. Makala inatupeleka kaunti ya Samburu nchini kenya kuona namna ngamia wanavyoboresha maisha ya wanawake na jamii kwa ujumla.Na mashinani inatupeleka katika ukanda wa Gaza ambapo ongezeko kubwa la utapiamlo miongoni mwa watoto na wanawake wajawazito na wanaonyonyesha ni tishio kubwa kwa afya zao. Shirika la Mpango wa chakula Duniani, WFP linahaha kuwasambazia lishe yenye virutubisho.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

    23 FEBRUARI 2024

    23 FEBRUARI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini DR Congo na hali ya msaada wa kibinadamu kwa wakimbizi wake. Pia tunakupeleka nchini Burundi kufuatilia kazi za makundi ya kijamii. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Ukraine tukielekea miaka mwili kamili ya vita nchini humo.Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kuhudumia watoto UNICEF na la mpango wa chakula duniani WFP leo yametoa wito wa kuchukuliwa hatua mara moja kuwalinda watoto na familia zao waliojikuta katikati ya machafuko yanayoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, huku lile la kuhudumia wakimbizi UNHCR likielezea wasiwasi mkubwa kuhusu mustakabali wa zaidi ya raia milioni 7 waliotawanywa na kuomba msaada zaidi kutoka jumuiya ya kimataifa.Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP Kanda ya Afrika, Ahunna Eziakonwa yuko ziarani nchini Burundi ambako amekutana na makundi mbalimbali ya kijamii na hata kufika mpaka wa Burundi na DRC kuona uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo. Makala inatupeleka katika chuo kikuu cha Nairobi Kenya ulikomalizika mkutano wa wanawake katika nyanja ya diplomasia. Huko viongozi wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Nairobi na Geneva Uswisi wamewasilisha mada mbele ya umati wa watu wakiwemo Mabalozi wastaafu na wa sasa wanaowakilisha mataifa yao Kenya kuhusu nafasi ya mwanamke katika diplomasia na kutimiza malengo ya maendeleo endelevu SDGs. Dkt. Elizabeth Kimani Murage anayefanyakazi na kituo cha utafiti na idadi ya watu Afrika kama mtafiti mkuu, ni miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo.Katika mashinani tukielekea miaka mwili kamili ya vita nchini Ukraine tutamsikia mmoja wa waathirika wa vita hiyo.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

    Hali DRC si hali tena, mashirika ya UN yataka msaada zaidi na ulinzi kwa raia

    Hali DRC si hali tena, mashirika ya UN yataka msaada zaidi na ulinzi kwa raia
    Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kuhudumia watoto UNICEF na la mpango wa chakula duniani WFP leo yametoa wito wa kuchukuliwa hatua mara moja kuwalinda watoto na familia zao waliojikuta katikati ya machafuko yanayoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, huku lile la kuhudumia wakimbizi UNHCR likielezea wasiwasi mkubwa kuhusu mustakbali wa zaidi ya raia milioni 7 waliotawanywa na kuomba msaada zaidi kutoka jumuiya ya kimataifa.Kwamujibu wa WFP na UNICEF idadi kuwa ya watu wakiwemo watoto wamejeruhiwa au kuawa karibu na makazi ya kambi za wakimbizi na yametoa wito kwa pande zote katika mzozo kuwalinda raia na kuruhusu mashirika ya misaada ya kibinadamu  kufanya kazi yao.Mashirika hayo yamesema mapigano ya sasa yamesababisha janga kubwa la kibinadamu na katika wiki mbili zilizopita yamesogea kilometa 25 mwagharibi mwa mji wa Goma kuelekea Sake ambako watoto na familia zao sasa wamezingirwa na mapigano.Mwakilishi wa UNICEF nchini DRC Grant Leaity amesema "Watoto nchini DRC wanahitaji amani sasa. Tunatoa wito kwa watoto kulindwa katika vita hivi na kukomesha ukatili huu kupitia juhudi mpya za kutafuta suluhu za kidiplomasia. Tuna wasiwasi mkubwa kuhusu usalama wa watoto na familia zao walio ndani na karibu na kambi za Goma.”Nalo shirika la UNHCR limesema  mapigano haya yamesababisha msongamano mkubwa wa watu kwenye kambi za wakimbizi ambazo tayari zimejaa pomoni watu waliofurushwa makwao. Watu zaidi ya 214,000 wamejiunga na watu wengine 500,000 ambao tayari walikimbia hadi maeneo ya karibu na Goma.Shirika hilo limesema linatiwa hofu kubwa kwani hadi sasa zaidi ya watu milioni 7 wametawanywa nchini DRC ukijumuisha na wengine nusu milioni ambao ni wakimbizi na wengi wanakabiliwa na changamoto za hali duni ya malazi, huduma mbovu za usafi na fursa finyu za kujipatia kipato.Ili kushughulikia changamoto hizo na nyingine nyingi za kibinadamu mwaka huu 2024 ombi la dola bilioni 2.6 lilizinduliwa wiki hii kusaidia watu milioni 8.7 wanaohitaji msaada wa kibinadamu DRC.Lakini jana pia UNHCR na washirika wake walizindua mkakati wa kikanda wa ulinzi na msaada kwa DRC unaohitaji dola milioni 668 kusaidia karibu wakimbizi milioni 1 na jamii zinazowahifadhi hasa nchini Angola, Burundi, Jamhuri ya Congo, Rwanda, Uganda, Tanzania na Zambia.

    Afghanistan: Watoto 683,000 wanufaika na madarasa ya elimu ya kijamii

    Afghanistan: Watoto 683,000 wanufaika na madarasa ya elimu ya kijamii
    Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF linafanya kila juhudi kuhakikisha watoto wanapata mahitaji yao ikiwemo elimu. Huko nchini Afghanistan shirika hilo limehakikisha zaidi ya wanafunzi 683,000 wanapata elimu wangali katika mazingira wanayoishi. Mtoto Khadija ni mmoja wa wanufaika wa madarasa ya elimu ya kijamii huko nchini Afghanistan. Kabla ya kuanza kwa programu hii inayofadhiliwa na UNICEF mtoto huyu na wenzake walikuwa hawaendi shule.Hapo awali, tulikuwa tunagombana na marafiki zangu sababu hatukujua kile kilicho bora. Mimi na marafiki zangu tulikuwa tunacheza sehemu yoyote ile hata kwenye uchafu, sababu hatukujua kuwa ni tatizo. Lakini baada ya kuandikishwa na kuanza kushiriki katika madarasa ya elimu ya kijamii, Khadija anasema anafurahia mambo anayojifunza shuleni na kushirikiana na wanafunzi wenzake darasani.Nina jisikia furaha na fahari. Napenda kujifunza hisabati, Dari, ujuzi wa kijamii na kuandika. Ninapokuja shuleni najifunza vitu vingi sana. Asilimia 60 ya wanufaika wa programu hii ya madarasa ya elimu ya kijamii inayotolewa kwa wanafunzi 683,000 nchini Afghanistani ni watoto wa kike.

    UNICEF Niger inawasaidia watoto kupona utapiamlo mkali

    UNICEF Niger inawasaidia watoto kupona utapiamlo mkali
    Nchini Niger shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto UNICEF linaendesha program mbalimbali za kusaidia kupambana na utapiamlo mkali kwa watoto kwa kutoa virutubisho, kuhakikisha kuna upatikanaji wa huduma bora za lishe na usaidizi wa unyonyeshaji. Mtoto Laoualy miezi miwili iliyopita alikuwa dhofuli hali, bibi yake Sahoura alikuwa na wasiwasi sana na kuamua kumkimbiza katika hospitali inayopatiwa usaidizi na UNICEF nchini Niger ambako huko aligundulika kuwa na utapiamlo mkali.“Mjukuu wangu alikuwa anaugua mafua akapata na homa, alikuwa hali kitu chochote na mdomo wake ukawa umevimba. Nilipowasili hospitali nilikuwa nimekata tamaa, alikuwa hawezi hata kusimama.”Kwasababu ya hali mbaya ya mtoto walilazwa. Pamoja na kupatiwa matibabu mengine hospitali hapo bibi Sahoura anasema mjukuu wake alianza kupatiwa maziwa ya matibabu kwa ajili ya utapiamlo. “Kidogo kidogo maziwa hayo ya matibabu kwa ajili ya utapiamlo yakaanza kurejesha hamu yake ya kula chakula. Na hata tuliporuhusiwa hospitali na kurejea nyumbani akawa anaendelea kula vyakula vingine pia.”Naam, miezi miwili baada ya mtoto Laoualy kuruhusiwa kutoka hospitali, hali yake ikoje? “Mjukuu wangu anaendelea vizuri, amepona na anajisikia vizuri” Mtoto Laoualy anaendelea kupatiwa maziwa ya matibabu. Maziwa haya ya matibabu hutumiwa kulisha watoto wadogo walio katika awamu ya 1 ya kupona kutokana na utapiamlo mkali.

    07 FEBRUARI 2024

    07 FEBRUARI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia vita vinavyoendelea katika ukanda wa Gaza, na afya ya watoto nchini Niger. Makala tunamulika kazi za vijana nchini Tanzania na mashinani tunakuletea ujumbe wa mhudumu wa afya nchini Afghanistan anayejitolea kuchochea afya bora kwa jamii.Vita huko Gaza kati ya Israel na wanamgambo wa kipalestina Hamas ikiingia mwezi wa tano hii leo na kuwa imesababisha vifo va wapalestina 27,585 na takribani 70,000 wamejeruhiwa, Mkuu wa masuala ya misaada ya dharura kwenye Umoja wa Mataifa amekaribisha dalili za mapema za uwezekano wa sitisho la mapigano linaloweza kufanikisha kuachiliwa huru kwa mateka wote waliosalia. Nchini Niger shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto UNICEF linaendesha program mbalimbali za kusaidia kupambana na utapiamlo mkali kwa watoto kwa kutoa virutubisho, kuhakikisha kuna upatikanaji wa huduma bora za lishe na usaidizi wa unyonyeshaji. Evarist Mapesa anasimulizi ya mmoja wa wanufaika wa huduma hizo za UNICEF. Makala inatupeleka Kilwa Masoko mkoani Lindi, kusini-,mashariki mwa Tanzania, katika bahari ya Hindi ambako Sawiche Wamunza, Afisa Mchambuzi wa Mawasiliano kutoka shirika la Umoja wa MAtaifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP nchini humo anazungumza na Nuru Mbaruku Ramadhani, mwenyekiti wa Kikundi kiitwacho Masoko 2 Peace Club, kinachonufaika na miradi inayotekelezwa na UNDP mkoani humo kama sehemu ya kuwezesha vijana kusongesha amani ili kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu SDGs, badala ya vijana kutumbukia kwenye misimamo mikali. Nuru anaanza kwa kuelezea sababu ya kuanzisha kikundi chao.Na mashinani tutaelekea nchini Afghanistan kushuhudia ni kwa jinsi gani wenyeji wanajitolea kuchochea afya bora kwa jamii.      Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

    Alvorada Social - Watoto faz turnê de três meses no Brasil; Projeto "Memórias do Clube da Esquina nas Escolas” acontece pela primeira vez em BH

    Alvorada Social - Watoto faz turnê de três meses no Brasil; Projeto "Memórias do Clube da Esquina nas Escolas” acontece pela primeira vez em BH

    Watoto: O Watoto é uma ONG em Uganda, no leste da África, que trabalha no resgate de órfãos e mulheres em situação de vulnerabilidade. Além de prestar um trabalho humanitário incrível, a instituição também apresenta o Coral de Crianças Watoto, que desde 1994 viaja o mundo compartilhando uma mensagem de esperança. Neste ano, o grupo retorna ao Brasil com o álbum “We Will Go” para uma turnê de três meses, e Belo Horizonte será uma das cidades visitadas. Com apresentações gratuitas, o grupo promete encantar o público. Para saber mais a respeito de locais e horários, além de outras informações sobre formas de ajudar a ONG, acesse o site da instituição.

    "Memórias do Clube da Esquina nas Escolas”: A iniciativa, realizada pelo Espaço Estação das Artes,  mostra toda a história do conjunto musical que despontou mundo afora de um jeito criativo e diferente. Na prática, a proposta é trabalhar o tema por meio de disciplinas como português, artes, música e história.ao longo do ano letivo. Por fim, os estudantes ainda vão participar de caravanas que irão desembarcar no bairro Santa Tereza, para que os alunos conheçam espaços e regiões que fizeram parte da trajetória do Clube da Esquina. Mais informações no site do BH Eventos

    See omnystudio.com/listener for privacy information.

    Joshua and Emma Quisenberry // African Gems

    Joshua and Emma Quisenberry // African Gems

    Joshua and Emma talk about the amazing work they are doing helping some of the most vulnerable disabled children in Uganda through holistic care. Seeking out their families and providing support for reunification when possible.

    - www.thegemfoundation.com
    - www.instagram.com/thegemfoundationuganda
    - www.facebook.com/TheGemFoundationUganda

    YouTube Version: www.youtube.com/RadicalLifestyle

    - Radical Lifestyle Instagram Click Here
    - Telegram channel and discussion: Click Here

    You can also follow Andrew and Daphne on their social media platforms:
    Andrew Kirk: Facebook | Instagram | Twitter | Parler
    Daphne Kirk: Facebook | Instagram | Twitter | Parler

    To support the channel: Click Here
    - UK only Donations here: Click Here

    Roland & Angela - Life in the War Room: Going From Loss to Legacy

    Roland & Angela - Life in the War Room: Going From Loss to Legacy

    Maybe you are familiar with the movie War Room that came out in 2015?  It was a film on prayer by the Kendrick Brothers (Fireproof, Courageous, Facing the Giants) that reached #1 in its second week.  My friends Roland and Angela Mitchell had no idea how much the film would impact their lives until the Kendrick Brothers came to their house and asked if they could use it as the location of their movie!

    What could seem to be a superficial, exciting opportunity actually held very deep, personal meaning to the Mitchell family. In this episode, Roland and Angela share about the devastating loss of their teenage son, Coleman, and how the movie and its message played a role in bringing redemption to both Coleman's story and their own.  They share how God has helped them go from loss to legacy as they allowed Him to continue to write His story. You will be impacted by their journey from pain to promise and from loss to legacy.

    Not only did God use the movie War Room but He partnered them with a ministry in Uganda that their son Coleman had intended to work with in the years to come. They now serve in leadership with that ministry as they steward Coleman's legacy and their own passion for the children of Uganda through a home they have built there to serve those in need.  You can learn more about Watoto here.

    With this episode focusing on navigating grief and going from loss to legacy, here are a few articles from Nathan's blog #TheBestViewInTown that may be of interest to you.

    1. Good Grief - The Pain That Heals All Others

    2. God Broke My Heart

    3. The Wound Is Where The Light Gets In

    As always you can find us at TheBestViewInTown.com or send us an email by clicking the link here.

    On this Episode:

    Guest: Roland & Angela Mitchell
    Host: Producer: Nathan Wesley Smith
    Cohost: Justin Porter

    Support the show

    We are on PATREON! Support the show by clicking here and get BONUS content!

    Join the Email Mailing list and have every new blog post and podcast sent to you directly by clicking here!

    Be sure to subscribe so you never miss the latest podcast and take a minute to rate the show on your favorite platform to help us get the show out to more people in more places. As always you can find us at TheBestViewInTown.com or send us an email by clicking the link here.

    Click the links to find Nathan's Music on Apple Music of Spotify
    Check out our YouTube Channel while you're at it!


    Ronie Kabwama (From Watoto To The Nations)

    Ronie Kabwama (From Watoto To The Nations)

    Ronie shares his story of losing both his parents to AIDS, joining a Watoto village and being raised to impact the nations which He is now doing as a worship leader.

    - www.limitlessworship.ke
    - www.youtube.com/limitlessworship

    YouTube Version: www.youtube.com/channel/UCQGRMndISia448cFZr_XLYw

    - Telegram channel and discussion: Click Here

    You can also follow Andrew and Daphne on their social media platforms:
    Andrew Kirk: Facebook | Instagram | Twitter | Parler
    Daphne Kirk: Facebook | Instagram | Twitter | Parler

    To support the channel: Click Here
    - UK only Donations here: Click Here

    Logo

    © 2024 Podcastworld. All rights reserved

    Stay up to date

    For any inquiries, please email us at hello@podcastworld.io