Logo

    kigoma

    Explore " kigoma" with insightful episodes like "KIGOMa: Mafunzo ya kilimo hifadhi kutoka FAO chaongeza mavuno mahindi kutoka magunia 4 hadi 45" and "08 MACHI 2024" from podcasts like ""Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu" and "Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu"" and more!

    Episodes (2)

    KIGOMa: Mafunzo ya kilimo hifadhi kutoka FAO chaongeza mavuno mahindi kutoka magunia 4 hadi 45

    KIGOMa: Mafunzo ya kilimo hifadhi kutoka FAO chaongeza mavuno mahindi kutoka magunia 4 hadi 45
    Sasa ni makala inayotupeleka mkoani Kigoma, kaskazini-magharibi mwa Tanzania ambako huko shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO limetekeleza kwa vitendo ujumbe wa mwaka huu wa siku ya wanawake duniani, Wekeza kwa Wanawake, Songesha Maendeleo, kwa kuwapatia mafunzo ya ufugaji bora wa kuku na mbuzi, halikadhalika kilimo hifadhi kisichoharibu mazingira. Sasa manufaa yako dhahiri kwani wanawake wameinuka kiuchumi. Miongoni mwao ni Hadija Alisido, mkazi wa kijiji Muhange, wilaya ya Kakonko. Katika makala hii inayoletwa kwako na Assumpta Massoi wa Idhaa hii, Hadija anaelezea alivyoinuliwa na FAO.

    08 MACHI 2024

    08 MACHI 2024
    Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Flora Nducha anamulika siku ya wanawake duniani kuanzia habari ya kwanza hadi ya mwisho maudhui yakiwa Wekeza kwa wanawake - songesha maendeleo.Katika kusherehekea siku ya wanawake duniani kote Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewapongeza wanawake na wasichana kwa kupata mafanikio makubwa na kuondoa vikwazo, kuvunja fikra potofu na kuchochea maendeleo kuelekea dunia yenye haki na usawa zaidi.Nchini Afrika Kusini katika jimbo la Western Cape kufuatia mafunzo kuhusu unyanyasaji wa kijinsia yaliyotolewa na kikundi cha wanawake cha Ilitha Labantu kwa vituo kadhaa vya polisi, sasa kuna ushahidi wa wazi kwamba vituo vya polisi vimeweka mazingira rafiki ya kuwasikiliza wanawake walionyanyaswa kuliko ilivyokuwa hapo awali. Anold Kayanda ameufuatilia mradi huo.Makala inatupeleka Kigoma nchini Tanzania kumsikia shuhuda Hadija Alisido ambaye amenufaika na miradi ya FAO.Mashinani tunabisha hodi Mwanza nchini Tanzania kupata maoni kuhusu siku ya wanawake duniani. Karibu!
    Logo

    © 2024 Podcastworld. All rights reserved

    Stay up to date

    For any inquiries, please email us at hello@podcastworld.io