Logo

    08 MACHI 2024

    swMarch 08, 2024
    What was the main topic of the podcast episode?
    Summarise the key points discussed in the episode?
    Were there any notable quotes or insights from the speakers?
    Which popular books were mentioned in this episode?
    Were there any points particularly controversial or thought-provoking discussed in the episode?
    Were any current events or trending topics addressed in the episode?

    About this Episode

    Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Flora Nducha anamulika siku ya wanawake duniani kuanzia habari ya kwanza hadi ya mwisho maudhui yakiwa Wekeza kwa wanawake - songesha maendeleo.Katika kusherehekea siku ya wanawake duniani kote Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewapongeza wanawake na wasichana kwa kupata mafanikio makubwa na kuondoa vikwazo, kuvunja fikra potofu na kuchochea maendeleo kuelekea dunia yenye haki na usawa zaidi.Nchini Afrika Kusini katika jimbo la Western Cape kufuatia mafunzo kuhusu unyanyasaji wa kijinsia yaliyotolewa na kikundi cha wanawake cha Ilitha Labantu kwa vituo kadhaa vya polisi, sasa kuna ushahidi wa wazi kwamba vituo vya polisi vimeweka mazingira rafiki ya kuwasikiliza wanawake walionyanyaswa kuliko ilivyokuwa hapo awali. Anold Kayanda ameufuatilia mradi huo.Makala inatupeleka Kigoma nchini Tanzania kumsikia shuhuda Hadija Alisido ambaye amenufaika na miradi ya FAO.Mashinani tunabisha hodi Mwanza nchini Tanzania kupata maoni kuhusu siku ya wanawake duniani. Karibu!

    Recent Episodes from Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

    12 MACHI 2024

    12 MACHI 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini India ambapo wahandisi wa usanifu majengo waliodhamiria kujenga mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kupunguza changamoto ya hewa ukaa katika sekta ya ujenzi kwa kutumia matofali ya matope. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani kama zifuatazo. Meli iliyosheheni misaada ya kibinadamu imeanza safari yake kutoka Cyprus kuelekea Gaza ikiwa na shehena ya tani 200 za misaada ya kuokoa maisha kwa ajili ya wananchi wa Gaza.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP hii leo linaonya kuwa litalazimika kusitisha misaada ya kuokoa maisha nchini Chad ifikapo mwezi ujao wa Aprili iwapo litakosa ufadhili wa haraka kwa ajili ya kusaidia wakimbizi. Na mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68, ukiendelea hapa jijini New York Marekani hii leo kutakuwa na mikutano ya kujadili mambo mbalimbali ikiwemo hali ya wanawake nchini Afghanistan, kuziba pengo la kujinsia kwenye elimu, athari za umaskini na uhalifu katika huduma ya utoaji mimba pamoja na mkutano wa kuangalia jinsi mabunge yanayozingatia jinsia katika kuendeleza usawa wa kijinsia ili kumaliza umaskini.Katika mashinani tunakuletea ujumbe wa Marynsia Mangu, kijana kutoka Tanzania na Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la Success Hands Tanzania anayeshiriki mkutano wa 68 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW68 hapa New York, Marekani akielezea matarajio yake kwenye mkutano huu.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

    Mlo shuleni umeongeza idadi ya wanafunzi wangu shule ya Salama: Mwalimu Beatrice Nyakoa Osaka

    Mlo shuleni umeongeza idadi ya wanafunzi wangu shule ya Salama: Mwalimu Beatrice Nyakoa Osaka
    Shule ya Salama iliyo katika eneo la Huruma karibu na mtaa wa mabanda wa Mathare jijini Nairobi Kenya hivi karibuni imeanza programu ya mlo shuleni kupitia mradi wa kampuni ya ‘Food for Education”. Hatua hiyo imenfa idadi ya wanafunzi wanaosoma shule hiyo kuongezeka kutoka 1, 900 hadi 2,300. Mlo shuleni ni moja ya masuala ambayo yanapigiwa debe kubwa na Umoja wa Mataifa sio tu kwa sababu ya kuhakikisha lishe bora kwa mamia ya maelfu ya wanafunzi ambao wengi hawawezi kupata mlo nyumbani bali pia kuongeza idadi ya watoto wanaohudhuria masomo. Stella Vuzo afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Kenya UNIS Nairobi amefunga safari hadi shuleni Salama na kuzungumza na mwalimu mkuu wa shule hiyo Beatrice Nyakoa Osaka anayeenza kwa kufafanua umuhimu wa mradi huo shuleni kwake hasa kutokana na eneo walipo.

    Mashambulizi na umwagaji damu vinaendelea Gaza licha ya kuanza kwa Ramadhan mauaji - Guterres

    Mashambulizi na umwagaji damu vinaendelea Gaza licha ya kuanza kwa Ramadhan mauaji - Guterres
    Leo ni mwanzo wa mwezi mktukufu wa Ramadhan ambapo Waislamu kote duniani husherehekea na kuchagiza tunu za amani, maridhiano na mshikamano lakini uhasama unaendelea hususani sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Gaza ambako mauaji , na mashambulizi hayajakoma amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza na waandishi wa habari mjini New York Marekani hii leo. Hivyo ndivyo alivyoanza Katibu Mkuu katika tarifa yake fupi kwa waandishi wa habari akikumbusha kuwa ni hivi majuzi tuliingia mwezi wa sita tangu shambulio la kigaidi la Hamas nchini Israel na mashambulizi mabaya ya Israel huko Gaza. Ameo leo ana ombi kubwa ambalo ni “kuheshimu dhamira ya Ramadhani kwa kunyamazisha mtutu wa bunduki na kuondoa vikwazo vyote ili kuhakikisha utoaji wa misaada ya kuokoa maisha kwa kasi na kiwango kikubwa kinachohitajika.”Pia ametaka wakati huohuo kwa kuzingatia dhamira ya Ramadhani kuwaachilia mateka wote wanaoshikiliwa mara moja. Katibu Mkuu ameonya kwamba “Macho yadunia yanatazama. Macho ya historia yanatazama. Hatuwezi kuyapa kisogo yanayoendelea ni lazima tuchukue hatua kuepusha vifo vinavyoweza kuzuilika.” Amesema Dunia imeshuhudia mwezi baada ya mwezi mauaji ya raia na uharibifu wa miundombinu ya raia kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea katika miaka yangu yote akiwa Katibu Mkuu. Na kwamba msaada wa kuokoa Maisha kwa raia Gaza unaingia kwa vikwazo vikbwa na wakati mwingine hauingii kabisa.Amesema hivi sasa Sheria ya kimataifa za kibinadamu ziko katika hali mbaya.Na tishio la Israel kushambulia Rafah zinaweza kuwatumbukiza kuzimu zaidi watu wa Gaza.Amesema pamoja na kwamba viongozi wa Dunia na wahudumu wa kibinadamu wamekuwa wakitoa wito wa kusitishwa mapigano wito mahsusi umetoka kwa familia za waathirika wa vita hivi. Sitasahau mikutano yangu pamoja nao na wamesimama kwenye jukwaa hili na kukuhutubia wameungana kwa ujasiri mkubwa na maumivu yasiyopimika. Familia za mateka wa Israeli ambao wameeleza mateso na uchungu wao na wameomba kuachiliwa mara moja kwa wapendwa wao. Pia alikutana na familia za waathirika wa Gaza ambazi zimeomba uhasama kutishishwa mara moja “Kama mmoja wa wanafamilia hao alisema, Hatuko hapa kwa ajili ya rambirambi. Hatupo hapa kwa ajili ya kuomba msamaha. Tuko hapa kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za haraka. Je, hili ni kubwa sana kuliomba? Ni lazima tusikilize na kutii sauti hizo.” Amesesisitiza Guterres. Pia amesema leo anatoa ombi la usitishaji uhasama Sudan kwa ajili ya Ramadhani na kukumbusha kwamba hivi karibuni mwezi Aprili kutakuwa na Sikukuu za Pasaka na sikukuu ya Wayahudi ya Passover hivyo huu ni wakati wa kuonyesha huruma, kuchukua hatua na kurejesha Amani.

    Mlo shuleni umeongeza idadi ya wanafunzi wangu shule ya Salama: Mwalimu Beatrice Osaka

    Mlo shuleni umeongeza idadi ya wanafunzi wangu shule ya Salama: Mwalimu Beatrice Osaka
    Shule ya Salama iliyo katika eneo la Huruma karibu na mtaa wa mabanda wa Mathare jijini Nairobi Kenya hivi karibuni imeanza programu ya mlo shuleni kupitia mradi wa kampuni ya ‘Food for Education”. Hatua hiyo imenfa idadi ya wanafunzi wanaosoma shule hiyo kuongezeka kutoka 1, 900 hadi 2,300. Mlo shuleni ni moja ya masuala ambayo yanapigiwa debe kubwa na Umoja wa Mataifa sio tu kwa sababu ya kuhakikisha lishe bora kwa mamia ya maelfu ya wanafunzi ambao wengi hawawezi kupata mlo nyumbani bali pia kuongeza idadi ya watoto wanaohudhuria masomo. Stella Vuzo afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Kenya UNIS Nairobi amefunga safari hadi shuleni Salama na kuzungumza na mwalimu mkuu wa shule hiyo Beatrice Nyakoa Osaka anayeenza kwa kufafanua umuhimu wa mradi huo shuleni kwake hasa kutokana na eneo walipo

    11 MACHI 2024

    11 MACHI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mkuu kuhusu mwezi mktukufu wa Ramadhan, na uwezeshaji wa wanawake wakulima nchini Malawai. Makala na mashinani tunakupeleka nchini Kenya, kulikoni? Leo ni mwanzo wa mwezi mktukufu wa Ramadhan ambapo Waislamu kote duniani husherehekea na kuchagiza tunu za amani, maridhiano na mshikamano lakini uhasama unaendelea hususani sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Gaza ambako mauaji , na mashambulizi hayajakoma amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza na waandishi wa habari mjini New York Marekani hii leo.Nchini Malawi Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya Kilimo IFAD unatekeleza mradi wa kuwasaidia wanawake wa vijijini kukabiliana na ukosefu wa usawa wa kijinsia na sasa wananachi wanafaidi matunda yake. Makala inatupeleka katika shule ya Salama iliyo katika eneo la Huruma karibu na mtaa wa mabanda wa Mathare jijini Nairobi Kenya hivi karibuni imeanza programu ya mlo shuleni kupitia mradi wa kampuni ya ‘Food for Education”. Hatua hiyo imenfa idadi ya wanafunzi wanaosoma shule hiyo kuongezeka kutoka 1, 900 hadi 2,300. Mlo shuleni ni moja ya masuala ambayo yanapigiwa debe kubwa na Umoja wa Mataifa sio tu kwa sababu ya kuhakikisha lishe bora kwa mamia ya maelfu ya wanafunzi ambao wengi hawawezi kupata mlo nyumbani bali pia kuongeza idadi ya watoto wanaohudhuria masomo.Na mashinanitunasalia nchini Kenya kumulika jinsi mradi wa FAO umemwezesha msichana mwenye ulemavu kuondokana na msongo wa mawazo na kisha kujikwamua kiuchumi.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

    IFAD: Mradi wa ukulima nchini Malawi waboresha maisha ya na usawa kijinsia katika jamii

    IFAD: Mradi wa ukulima nchini Malawi waboresha maisha ya na usawa kijinsia katika jamii
    Nchini Malawi Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya Kilimo IFAD unatekeleza mradi wa kuwasaidia wanawake wa vijijini kukabiliana na ukosefu wa usawa wa kijinsia na sasa wananachi wanafaidi matunda yake. Mradi huo uitwao TRADE ulioanzishwa mwaka 2022 na serikali ya Malawi kwa kushirikiana na IFAD inalenga kubadilisha kilimo kupitia mpango wake wa Mseto na Ujasiriamali. Amos Mailosi ni Afisa Mazingira wa kanda Mabadiliko ya Tabianchi wa mradi huo wa TRADE na anasema jambo muhimu katika mradi wao ni kuhakikisha familia zinafanya kazi na kufikia maamuzi pamoja. “Moja ya eneo muhimu katika programu yetu ya TRADE ni kuhamasisha suala la ushirikishwaji wa kijinsia ndani ya jamii. Kwa hivyo, tunajaribu kuwawezesha wanawake na wanaume, na wavulana na wasichana, kushiriki kwa usawa katika afua. Ili kwa pamoja waweze kutambua umuhimu wa kufanya maamuzi ya pamoja katika ngazi ya kaya.”Kwa miaka mwili sasa mafanikio yameanza kuoneskana, na mmoja wa wanufaika hao ni Alefu Ofesa na mume wake Lloyd ambao wamekuwa wakulima kwa miaka 20 lakini kwa takriban miaka miwili wamebadili kilimo kuwa biashara. Mabadiliko haya yamefuatitia Alefa na wanawake wenzake kijijini kupatiwa Msaada na mafunzo ya mbinu mpya za kilimo ambazo zimewasaidia kukabiliana na mvua zisizokuwa na uhakika katika ukanda huo. “Mradi huu umekuwa ukihimiza wanawake kushiriki katika kilimo. Kwa ujuzi na maarifa tuliyopatiwa tuna uhakika kuhusu kile kinachohitajika kufanywa ili kuboresha uzalishaji, kwa mfano upandaji kwa kutumia mistari miwili. Wanawake wengi hapa sasa ni wataalam wa shughuli za kilimo na kwa sababu ya faida wanazopata, wengi wametambua umuhimu wa kujiunga pamoja.”Alefa amepanga kutumia mapato ya ziada wanayopata kwa ajili ya kuwapatia elimu watoto wao na kununua kigari cha ng'ombe kwa ajili ya usafiri. Sio tu kwamba familia yake sasa ina chakula cha kutosha kwa mwaka mzima, lakini sasa anaweza pia kuuza sehemu ya kile anachovuna, na anapanga kupanua biashara yake ili kuuza kwenye masoko katika vijiji vya jirani.

    KIGOMa: Mafunzo ya kilimo hifadhi kutoka FAO chaongeza mavuno mahindi kutoka magunia 4 hadi 45

    KIGOMa: Mafunzo ya kilimo hifadhi kutoka FAO chaongeza mavuno mahindi kutoka magunia 4 hadi 45
    Sasa ni makala inayotupeleka mkoani Kigoma, kaskazini-magharibi mwa Tanzania ambako huko shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO limetekeleza kwa vitendo ujumbe wa mwaka huu wa siku ya wanawake duniani, Wekeza kwa Wanawake, Songesha Maendeleo, kwa kuwapatia mafunzo ya ufugaji bora wa kuku na mbuzi, halikadhalika kilimo hifadhi kisichoharibu mazingira. Sasa manufaa yako dhahiri kwani wanawake wameinuka kiuchumi. Miongoni mwao ni Hadija Alisido, mkazi wa kijiji Muhange, wilaya ya Kakonko. Katika makala hii inayoletwa kwako na Assumpta Massoi wa Idhaa hii, Hadija anaelezea alivyoinuliwa na FAO.

    08 MACHI 2024

    08 MACHI 2024
    Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Flora Nducha anamulika siku ya wanawake duniani kuanzia habari ya kwanza hadi ya mwisho maudhui yakiwa Wekeza kwa wanawake - songesha maendeleo.Katika kusherehekea siku ya wanawake duniani kote Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewapongeza wanawake na wasichana kwa kupata mafanikio makubwa na kuondoa vikwazo, kuvunja fikra potofu na kuchochea maendeleo kuelekea dunia yenye haki na usawa zaidi.Nchini Afrika Kusini katika jimbo la Western Cape kufuatia mafunzo kuhusu unyanyasaji wa kijinsia yaliyotolewa na kikundi cha wanawake cha Ilitha Labantu kwa vituo kadhaa vya polisi, sasa kuna ushahidi wa wazi kwamba vituo vya polisi vimeweka mazingira rafiki ya kuwasikiliza wanawake walionyanyaswa kuliko ilivyokuwa hapo awali. Anold Kayanda ameufuatilia mradi huo.Makala inatupeleka Kigoma nchini Tanzania kumsikia shuhuda Hadija Alisido ambaye amenufaika na miradi ya FAO.Mashinani tunabisha hodi Mwanza nchini Tanzania kupata maoni kuhusu siku ya wanawake duniani. Karibu!

    Ukatili dhidi ya wanawake Afrika kusini: Polisi 'wanolewa' sasa mambo ni shwari

    Ukatili dhidi ya wanawake Afrika kusini: Polisi 'wanolewa' sasa mambo ni shwari
    Nchini Afrika Kusini katika jimbo la Western Cape kufuatia mafunzo kuhusu unyanyasaji wa kijinsia yaliyotolewa na kikundi cha wanawake cha Ilitha Labantu kwa vituo kadhaa vya polisi, sasa kuna ushahidi wa wazi kwamba vituo vya polisi vimeweka mazingira rafiki ya kuwasikiliza wanawake walionyanyaswa kuliko ilivyokuwa hapo awali. Anold Kayanda ameufuatilia mradi huo. Karibu Anold utueleze zaidi.(Taarifa ya Anold Kayanda)Asante sana Flora Nducha. Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake (UN Women) linasema kiwango cha unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana nchini Afrika Kusini ni miongoni mwa viwango vya juu zaidi duniani na wanafafanua wakisema kwamba mwanamke mmoja kati ya watano walio katika uhusiano amepitia ukatili wa kimwili uliofanywa na mpenzi wake.Wengi zaidi wameteseka na aina nyingine za vurugu kutoka kwa wanaume wanaowajua na wasiowajua lakini changamoto zaidi ni namna ya kuyashughulikia masuala haya kwani matukio mengi ya unyanyasaji hayaripotiwi kwa mamlaka kutokana na imani ndogo kwa vyombo vya sheria.Ella Mangisa, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo la Ilitha Labantu  anasema ulikuwa unakuta mwanamke anayekimbia hali ya vurugu, akifika polisi ataambiwa arudi nyumbani akaelewane na mnyanyasaji wake au kuambiwa haya ni masuala ya kibinafsi wanayohitaji kutatua wao wenyewe."Kupitia ushirikiano na UN Women na wadau wengine ndipo Ilitha Labantu mwaka 2021 ilizindua mpango wa kufanya kazi na Huduma ya Polisi ya Afrika Kusini (SAPS) kuwaelimisha maafisa kufanya kazi na waathirika wa ukatili wa kijinsia. Mpango umetekelezwa katika vituo 75 vya polisi huko Cape Metro na Cape Winelands katika Mkoa wa Western Cape.Ilitha Labantu inapanga kupanua zaidi mpango huo na kushirikisha mashirika mengine yenye utaalamu tofauti. Shirika hilo pia linatarajia kujumuisha maudhui ya mafunzo yao katika mtaala wa vyuo vya polisi kote nchini Afrika Kusini.

    Kuwekeza kwa wanawake ni jawabu sahihi - Guterres

    Kuwekeza kwa wanawake ni jawabu sahihi - Guterres
    Katika kusherehekea siku ya wanawake duniani kote Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewapongeza wanawake na wasichana kwa kupata mafanikio makubwa na kuondoa vikwazo, kuvunja fikra potofu na kuchochea maendeleo kuelekea dunia yenye haki na usawa zaidi.  Leah Mushi na maelezo zaidi.Katika ujumbe wake kwa siku hii Katibu Mkuu Guterres amesema “Pamoja na juhudi wanazozifanya kila siku bado wanakabiliwa na vikwazo vikubwa. Mabilioni ya wanawake na wasichana wanakabiliwa na kuenguliwa, ukosefu wa haki na ubaguzi, ilhali janga lililojikita la ukatili dhidi ya wanawake lilikimomonyoa ubinamu.”Amesema ni vyema kuongeza juhudi ikiwemo za kisheria katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili wanawake kwani kwa kasi ya sasa itachukua miaka miatatu kupata usawa.Akieleza nini kifanyike amesema “ tunapaswa kuwekeza kwenye miradi ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na kuchochea ujumuishaji wanawake na uongozi wa wanawake kwenye uchumi, teknolojia za kidijitali, ujenzi wa amani na hatua kwa tabianchi.Yote hii inategemea kupatikana kwa fedha kwa ajili ya maendeleo endelevu ili nchi ziwe na fedha za kuwekeza kwa wanawake na wasichana.”Kauli mbiu ya siku ya wanawake kwa mwaka huu ni wekeza kwa wanawake ili kuharakisha maendeleo na Mkuu huyo wa umoja wa Mataifa amesema inatukumbusha kuwa kutokomeza mfumo dume kunahitaji kuweko kwa fedha mezani.“Tunahitaji pia kuongeza idadi ya wanawake viongozi kwenye sekta ya biashara, Benki Kuu na Wizara za Fedha. Hii inaweza kusaidia kuchochea uwekezaji kwenye sera na miradi inayokidhi mahitaji ya wanawake na wasichana.Haki za wanawake zimedhihirisha kuwa njia ya haki ya jamii zenye haki, amani na ustawi. Hii ni vema kwetu sote. “Kwa Pamoja, hebu na tuchukue hatua za haraka kufanya kuwa halisia.”Usawa kwa woteNalo shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women linaadhimisha siku hii kwa kufanya mkutano mkubwa katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani utakao wakutanisha pamoja viongozi wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa masuala ya wanawake. UN Women wamesema katika mwaka huu ambapo karibu nusu ya watu duniani wanaishi katika nchi zinazoshiriki katika uchaguzi, Siku hii ya Kimataifa ya Wanawake ni fursa muhimu ya kufafanua siku zijazo tunazotaka.Wakati mizozo, mabadiliko ya tabianchi na jamii zenye mgawanyiko zikididimiza miongo kadhaa ya maendeleo katika usawa wa kijinsia, UN Women inatoa wito waku "Wekeza kwa wanawake ili Kuharakisha Maendeleo" ili hatimae dunia iweze kufikia faida ya usawa wa kijinsia kwa wote.
    Logo

    © 2024 Podcastworld. All rights reserved

    Stay up to date

    For any inquiries, please email us at hello@podcastworld.io