Logo

    wanawake

    Explore "wanawake" with insightful episodes like "11 MACHI 2024", "IFAD: Mradi wa ukulima nchini Malawi waboresha maisha ya na usawa kijinsia katika jamii", "Wanawake na wasichana wakiwezeshwa jamii zinanufaika - Wanabiashara Kenya", "JINSI MALEZI NA JAMII HUATHIRI MITAZAMO YA KIJINSIA KATIKA UCHAGUZI WA KAZI ZA KITAALUMA" and "Utangulizi" from podcasts like ""Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu", "Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu", "Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu", "Mwanamke wa kazi's Podcast" and "Mwanamke wa kazi's Podcast"" and more!

    Episodes (8)

    11 MACHI 2024

    11 MACHI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mkuu kuhusu mwezi mktukufu wa Ramadhan, na uwezeshaji wa wanawake wakulima nchini Malawai. Makala na mashinani tunakupeleka nchini Kenya, kulikoni? Leo ni mwanzo wa mwezi mktukufu wa Ramadhan ambapo Waislamu kote duniani husherehekea na kuchagiza tunu za amani, maridhiano na mshikamano lakini uhasama unaendelea hususani sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Gaza ambako mauaji , na mashambulizi hayajakoma amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza na waandishi wa habari mjini New York Marekani hii leo.Nchini Malawi Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya Kilimo IFAD unatekeleza mradi wa kuwasaidia wanawake wa vijijini kukabiliana na ukosefu wa usawa wa kijinsia na sasa wananachi wanafaidi matunda yake. Makala inatupeleka katika shule ya Salama iliyo katika eneo la Huruma karibu na mtaa wa mabanda wa Mathare jijini Nairobi Kenya hivi karibuni imeanza programu ya mlo shuleni kupitia mradi wa kampuni ya ‘Food for Education”. Hatua hiyo imenfa idadi ya wanafunzi wanaosoma shule hiyo kuongezeka kutoka 1, 900 hadi 2,300. Mlo shuleni ni moja ya masuala ambayo yanapigiwa debe kubwa na Umoja wa Mataifa sio tu kwa sababu ya kuhakikisha lishe bora kwa mamia ya maelfu ya wanafunzi ambao wengi hawawezi kupata mlo nyumbani bali pia kuongeza idadi ya watoto wanaohudhuria masomo.Na mashinanitunasalia nchini Kenya kumulika jinsi mradi wa FAO umemwezesha msichana mwenye ulemavu kuondokana na msongo wa mawazo na kisha kujikwamua kiuchumi.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

    IFAD: Mradi wa ukulima nchini Malawi waboresha maisha ya na usawa kijinsia katika jamii

    IFAD: Mradi wa ukulima nchini Malawi waboresha maisha ya na usawa kijinsia katika jamii
    Nchini Malawi Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya Kilimo IFAD unatekeleza mradi wa kuwasaidia wanawake wa vijijini kukabiliana na ukosefu wa usawa wa kijinsia na sasa wananachi wanafaidi matunda yake. Mradi huo uitwao TRADE ulioanzishwa mwaka 2022 na serikali ya Malawi kwa kushirikiana na IFAD inalenga kubadilisha kilimo kupitia mpango wake wa Mseto na Ujasiriamali. Amos Mailosi ni Afisa Mazingira wa kanda Mabadiliko ya Tabianchi wa mradi huo wa TRADE na anasema jambo muhimu katika mradi wao ni kuhakikisha familia zinafanya kazi na kufikia maamuzi pamoja. “Moja ya eneo muhimu katika programu yetu ya TRADE ni kuhamasisha suala la ushirikishwaji wa kijinsia ndani ya jamii. Kwa hivyo, tunajaribu kuwawezesha wanawake na wanaume, na wavulana na wasichana, kushiriki kwa usawa katika afua. Ili kwa pamoja waweze kutambua umuhimu wa kufanya maamuzi ya pamoja katika ngazi ya kaya.”Kwa miaka mwili sasa mafanikio yameanza kuoneskana, na mmoja wa wanufaika hao ni Alefu Ofesa na mume wake Lloyd ambao wamekuwa wakulima kwa miaka 20 lakini kwa takriban miaka miwili wamebadili kilimo kuwa biashara. Mabadiliko haya yamefuatitia Alefa na wanawake wenzake kijijini kupatiwa Msaada na mafunzo ya mbinu mpya za kilimo ambazo zimewasaidia kukabiliana na mvua zisizokuwa na uhakika katika ukanda huo. “Mradi huu umekuwa ukihimiza wanawake kushiriki katika kilimo. Kwa ujuzi na maarifa tuliyopatiwa tuna uhakika kuhusu kile kinachohitajika kufanywa ili kuboresha uzalishaji, kwa mfano upandaji kwa kutumia mistari miwili. Wanawake wengi hapa sasa ni wataalam wa shughuli za kilimo na kwa sababu ya faida wanazopata, wengi wametambua umuhimu wa kujiunga pamoja.”Alefa amepanga kutumia mapato ya ziada wanayopata kwa ajili ya kuwapatia elimu watoto wao na kununua kigari cha ng'ombe kwa ajili ya usafiri. Sio tu kwamba familia yake sasa ina chakula cha kutosha kwa mwaka mzima, lakini sasa anaweza pia kuuza sehemu ya kile anachovuna, na anapanga kupanua biashara yake ili kuuza kwenye masoko katika vijiji vya jirani.

    Wanawake na wasichana wakiwezeshwa jamii zinanufaika - Wanabiashara Kenya

    Wanawake na wasichana wakiwezeshwa jamii zinanufaika - Wanabiashara Kenya
    Wiki hii Ijumaa tarehe 8 Machi 2024, ulimwengu utaadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambapo mwaka huu ina maudhui “Wekeza kwa wanawake: Harakisha maendeleo,” lakini Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN Women linasema ni dhahiri kwamba ulimwengu bado unakabiliwa na migogoro mingi, kuanzia mizozo ya kijiografia hadi viwango vya umaskini vinavyoongezeka, ukosefu wa usawa na kuongezeka kwa athari za mabadiliko ya tabianchi.Kwa kuwekeza kwa wanawake, tunaweza kuibua mabadiliko na kuharakisha mpito kuelekea dunia yenye afya, usalama na usawa zaidi kwa wote. Nchini Kenya tunakutana na mama mjasiriamali ambaye alianza kwa kufanya kazi na shirika lisilo la kiserikali liitwalo Sime Food, ambalo linahusika na kilimo endelevu, lishe bora, na stadi za biashara ndogo ndogo ili wawe na maarifa na ujuzi unaohitajika ili kupatia familia zao lishe bora mwaka mzima na kuuza masalio ili kusaidia kulipia mahitaji mengine ya kaya. Baada ya kupata mafunzo hayo na fedha za kuanzisha biashara zake, Lucy anachochea kinamama na vijana wa kike wajiunge naye katika sekta ya biashara ili waweze kujikwamua kiuchumi. Selina Jerobon wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amefuatilia na kutuandalia makala hii.

    JINSI MALEZI NA JAMII HUATHIRI MITAZAMO YA KIJINSIA KATIKA UCHAGUZI WA KAZI ZA KITAALUMA

    JINSI MALEZI NA JAMII HUATHIRI MITAZAMO YA KIJINSIA KATIKA UCHAGUZI WA KAZI ZA KITAALUMA

    Katika kipindi hiki utasikia maoni ya watu mbalimbali juu ya mitazao yao kuhusu kazi za kike na za kiume. Pia tumeongea na watu ambao baadhi ya watu katika jamii inawatazama kama wanafanya kazi za jinsia nyingine  pia wadau na wataalamu wa maswala ya kijinsia wakielezea changamoto ya kugawa kazi za kitaaluma kijinsi na nini cha kufanya kuondoa mgawanyo huu.  

    Logo

    © 2024 Podcastworld. All rights reserved

    Stay up to date

    For any inquiries, please email us at hello@podcastworld.io