Logo

    wakulima

    Explore " wakulima" with insightful episodes like "11 MACHI 2024", "IFAD: Mradi wa ukulima nchini Malawi waboresha maisha ya na usawa kijinsia katika jamii", "16 FEBRUARI 2024", "14 FEBRUARI 2024" and "26 JANUARI 2024" from podcasts like ""Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu", "Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu", "Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu", "Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu" and "Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu"" and more!

    Episodes (5)

    11 MACHI 2024

    11 MACHI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mkuu kuhusu mwezi mktukufu wa Ramadhan, na uwezeshaji wa wanawake wakulima nchini Malawai. Makala na mashinani tunakupeleka nchini Kenya, kulikoni? Leo ni mwanzo wa mwezi mktukufu wa Ramadhan ambapo Waislamu kote duniani husherehekea na kuchagiza tunu za amani, maridhiano na mshikamano lakini uhasama unaendelea hususani sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Gaza ambako mauaji , na mashambulizi hayajakoma amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza na waandishi wa habari mjini New York Marekani hii leo.Nchini Malawi Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya Kilimo IFAD unatekeleza mradi wa kuwasaidia wanawake wa vijijini kukabiliana na ukosefu wa usawa wa kijinsia na sasa wananachi wanafaidi matunda yake. Makala inatupeleka katika shule ya Salama iliyo katika eneo la Huruma karibu na mtaa wa mabanda wa Mathare jijini Nairobi Kenya hivi karibuni imeanza programu ya mlo shuleni kupitia mradi wa kampuni ya ‘Food for Education”. Hatua hiyo imenfa idadi ya wanafunzi wanaosoma shule hiyo kuongezeka kutoka 1, 900 hadi 2,300. Mlo shuleni ni moja ya masuala ambayo yanapigiwa debe kubwa na Umoja wa Mataifa sio tu kwa sababu ya kuhakikisha lishe bora kwa mamia ya maelfu ya wanafunzi ambao wengi hawawezi kupata mlo nyumbani bali pia kuongeza idadi ya watoto wanaohudhuria masomo.Na mashinanitunasalia nchini Kenya kumulika jinsi mradi wa FAO umemwezesha msichana mwenye ulemavu kuondokana na msongo wa mawazo na kisha kujikwamua kiuchumi.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

    IFAD: Mradi wa ukulima nchini Malawi waboresha maisha ya na usawa kijinsia katika jamii

    IFAD: Mradi wa ukulima nchini Malawi waboresha maisha ya na usawa kijinsia katika jamii
    Nchini Malawi Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya Kilimo IFAD unatekeleza mradi wa kuwasaidia wanawake wa vijijini kukabiliana na ukosefu wa usawa wa kijinsia na sasa wananachi wanafaidi matunda yake. Mradi huo uitwao TRADE ulioanzishwa mwaka 2022 na serikali ya Malawi kwa kushirikiana na IFAD inalenga kubadilisha kilimo kupitia mpango wake wa Mseto na Ujasiriamali. Amos Mailosi ni Afisa Mazingira wa kanda Mabadiliko ya Tabianchi wa mradi huo wa TRADE na anasema jambo muhimu katika mradi wao ni kuhakikisha familia zinafanya kazi na kufikia maamuzi pamoja. “Moja ya eneo muhimu katika programu yetu ya TRADE ni kuhamasisha suala la ushirikishwaji wa kijinsia ndani ya jamii. Kwa hivyo, tunajaribu kuwawezesha wanawake na wanaume, na wavulana na wasichana, kushiriki kwa usawa katika afua. Ili kwa pamoja waweze kutambua umuhimu wa kufanya maamuzi ya pamoja katika ngazi ya kaya.”Kwa miaka mwili sasa mafanikio yameanza kuoneskana, na mmoja wa wanufaika hao ni Alefu Ofesa na mume wake Lloyd ambao wamekuwa wakulima kwa miaka 20 lakini kwa takriban miaka miwili wamebadili kilimo kuwa biashara. Mabadiliko haya yamefuatitia Alefa na wanawake wenzake kijijini kupatiwa Msaada na mafunzo ya mbinu mpya za kilimo ambazo zimewasaidia kukabiliana na mvua zisizokuwa na uhakika katika ukanda huo. “Mradi huu umekuwa ukihimiza wanawake kushiriki katika kilimo. Kwa ujuzi na maarifa tuliyopatiwa tuna uhakika kuhusu kile kinachohitajika kufanywa ili kuboresha uzalishaji, kwa mfano upandaji kwa kutumia mistari miwili. Wanawake wengi hapa sasa ni wataalam wa shughuli za kilimo na kwa sababu ya faida wanazopata, wengi wametambua umuhimu wa kujiunga pamoja.”Alefa amepanga kutumia mapato ya ziada wanayopata kwa ajili ya kuwapatia elimu watoto wao na kununua kigari cha ng'ombe kwa ajili ya usafiri. Sio tu kwamba familia yake sasa ina chakula cha kutosha kwa mwaka mzima, lakini sasa anaweza pia kuuza sehemu ya kile anachovuna, na anapanga kupanua biashara yake ili kuuza kwenye masoko katika vijiji vya jirani.

    16 FEBRUARI 2024

    16 FEBRUARI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa usalama unaofanyika mjini Munich Ujerumani, na elimu kwa watoto katika mzozo nchini Afghanistan. Makala tunasikia ujumbe kuhusu matatizo kwa upande wa taaluma ya utangazaji wa redio. Mashinani tunasikia ujumbe wa mkulima nchini Kenya.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo katika mkutano wa usalama unaofanyika mjini Munich Ujerumani ametoa wito wa kuwepo utaratibu wa kimataifa ambao unafanya kazi kwa kila mtu.Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF linafanya kila juhudi kuhakikisha watoto wanapata mahitaji yao ikiwemo elimu. Huko nchini Afghanistan shirika hilo limehakikisha zaidi ya wanafunzi 683,000 wanapata elimu wangali katika mazingira wanayoishi. Katika makala na ikiwa wiki hii ulimwengu umeadhimisha Siku ya redio Duniani, Mwanahabari gwiji wa siku nyingi nchini Tanzania Rose Haji anakubaliana na mtazamo wa Umoja wa Mataifa kuwa redio bado ni chombo muhimu sana katika mawasiliano ya ulimwengu lakini anaona kwamba kwa upande wa taaluma ya utangazaji wa redio kuna tatizo.Mashinani tunakuletea ujumbe wa Agnes, mwanamke mkulima kutoka Kenya ambaye alikuwa anategemea chakula cha msaada kutoka Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP lakini leo, kupitia mtaro wake wa maji inayopeleka maji kwa shamba lake, anavuna mazao yake ya kutosha familia yake na ameweza kujimudu kimaisha kwa kuuza masalio.Mwenyeji wako ni Evarist Mapesa, karibu!

    14 FEBRUARI 2024

    14 FEBRUARI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na jinsi amabvyo watu kote ulimwenguni wanavyokabiliwa na njaa kali inayochochewa na migogoro ya silaha. Makala tuansalia na mada ya mwaka huu wa siku ya redio na mashinani tunakupeleka nchini Chad, kulikoni?Madaktari wa Umoja wa Mataifa leo wamesema wanahofia janga la kibinadamu lisiloelezeka endapo uvamizi kamili wa jeshi la Israeli utatokea Rafah kusini mwa Gaza ambako maelfu ya maelfu ya watu wamekimbilia tangu kuzuka kwa mzozo huu mpya Oktoba 7 mwaka jana.Takriban watu milioni 258 katika nchi na maeneo 58 ulimwenguni wanakabiliwa na njaa kali inayochochewa na migogoro ya silaha, majanga ya kiuchumi, mabadiliko ya tabianchi, umaskini na ukosefu wa usawa, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO na kutaka wadau kuangalia upya mtindo wa ufadhili. Katika makala, licha ya redio ambacho ni chombo cha kuaminiwa kwa miaka mingi katika usambazaji wa taarifa, kukabiliwa na changamoto nyingi katika nyakati hizi ambazo kuna utitiri wa teknolojia za usambazaji wa habari, bado inaonekana watu wana imani kubwa na chombo hiki kwa sababu mbalimbali. Wachache kati ya wengi, ni wadau hawa tuliozungumza kutoka Afrika Mashariki.Mashinani tunakuletea ujumbe wa mwanamke dereva wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP anayeendesha gari muhimu aina ya sherps lililoundwa kumudu hali tofautitofauti za barabara na hata mito yenye vina vifupi ambalo husaidia kutoa huduma kwa namna yoyote.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

    26 JANUARI 2024

    26 JANUARI 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia maamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ vitendo vya mauaji ya kimbari katika mashambulizi ya Israel dhidi ya wapalestina huko Gaza. Pia tunamulika viwanda vya nishati safi ulimwenguni, makala ikitupeleka nchini India. Mashinani tnakuletea ujumbe wa mhamiaji ambaye ni mchezaji wa musiki, mwalimu na rafiki nchini Burundi.Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ hii leo imeamua kuwa Israel lazima ichukue hatua zote za kuzuia vitendo vya mauaji ya kimbari katika mashambulizi yake dhidi ya wapalestina huko, Gaza, uamuzi unaofuatia shauri lililowasilishwa na Afrika Kusini la kutaka Mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa ichukue hatua za awali kwa mujibu wa Mkataba wa kimataifa wa kuepusha mauaji ya kimbari wa mwaka 1948. Assumpta Massoi amefuatilia na kuandaa taarifa ifuatayo.     Kilimo ni moja ya shughuli za kibinadamu zinazochangia katika uchafuzi wa hewa. Kwa kulitambua hilo, FAO kote ulimwenguni inachagiza kile inachokiita kwa lugha ya kiingereza Bioeconomy yaani uchumi ambao msingi wake unatokana na matumizi ya rasilimali za kibayolojia zinazopatikana kwenye mazingira; kwa mfano kurejesha taka katika uzalishaji wa nishati safi, mbadala wa mafuta ya kisukuku. Kupitia harakati hizo, FAO inasaidia wakulima kuongeza mapato, kupunguza uzalishaji wa hewa chafuzi na kuchangia kupunguza taka ulimwenguni kwa kubadilisha mifumo ya zamani ya kilimo ambayo ilikuwa inachangia kuharibu mazingira.Na makala ikiwa leo ni maadhimisho ya kwanza kabisa ya siku ya kimataifa ya nishati safi nakupeleka Tanzania kuangazia juhudi zinazofanyika kuhamasisha umma kuhamia kwenye nishati safi au jadidifu kutimiza lengo namba 7 la maendeleo endelevu SDGs. Vijana wako msitari wa mbele katika harakati hizo na miongoni mwao ni Nuzulack Dausen mwanzilishi wa Jukwaa la kidijitali la Jiko point linaloendesha kipindi cha mwanaume jikoni kupitia mtandao wa Youtube. Amezungumza hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Stella Vuzo afisa habari wa Umoja wa Mataifa na kumfafanulia wanavyochangia katika kufanikisha lengo la maendeleo endelevu la Umoja wa Mataifa      kuhusu nishati safi . Mashinani tutaelekea katika Jiji la Bujumbura nchini Burundi kumsikia mhamiaji ambaye ni mchezaji wa musiki, mwalimu na rafiki.      Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    Logo

    © 2024 Podcastworld. All rights reserved

    Stay up to date

    For any inquiries, please email us at hello@podcastworld.io